Saturday, 6 March 2010

Kwa mara ya kwanza kutokea tukio la kuuliwa kikatili mtoto na mama yake mzazi kwa kuchomwa visu sehemu mbali mbali za mwili wake.
Tukio hilo limetokea katika wilaya ya Micheweni kisiwani Pemba ambapo tukio hilo limekuwa likiwatia hudhuni wakaazi wengi wa maeneo hayo.
Anaedaiwa kuuwa watu hao anadaiwa kuwa ni bada wa mtoto ambae alikuwa anaishi nae kinyumba

Sunday, 14 February 2010

Kiongozi wa kambi ya upizani AbuuBakari Khamis Bakar ambae ndie alipeleka mswaada wa maridhiano katika baraza la wawakilishi ambapo mswaada huo ulipelekea kubalishwa kwa vifungu mbali mbali vya sheria ikiwemo ni pamoja na makamo wa raisi kutoka katika majimbo ambayo yanaongozwa na wakilishi wengfi majimboni.

HUKUMU YA KUSHEREHEKEA VALENTINE DAY SIKU YA WAPENDANAO KILA MWAKA FEBUARY 14.
Valentine (Siku Ya Wapendanao) Na Hukumu Ya Kuisherehekea


http://www.alhidaaya.com/
BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu was Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa ‘Aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa Ba’ad,
Allaah سبحانه وتعالى Ametuchagulia dini ya Kiislamu ambayo ndio dini ya haki na Hatokubali dini yoyote nyingine kama Anavyosema:
((وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الإِسْلاَمِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ))
((Na anayetafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasirika)) [Al-'Imraan:85]
Na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ametuambia kuwa kutakua na makundi katika ummah wake ambao watawafuata maadui wa Allaah سبحانه وتعالى katika desturi na mila zao kama ifuatavyo:
((ستتبعون سنن من كان قبلكم شبراً بشبر وذراعاً بذراع حتى لو دخلوا جحر ضب لدخلتموه)) قالوا: أتراهم اليهود والنصارى؟ قال: ((فمن إذن؟)) البخاري ومسلم
((Mtafuata nyendo za wale waliokuja kabla yenu hatua kwa hatua mpaka itafika hadi wakiingia katika shimo la kenge, na nyinyi mtaingia pia)) Wakasema (Maswahaba): Ewe Mtume! Je, unamaanisha Mayahudi na Manaswara? Akasema: ((Hivyo nani basi mwengine?)) Al-Bukhariy na Muslim
Maneno hayo aliyoyasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hakika yamesadikika kwani tunaona jinsi gani Waislamu siku hizi wanavyoigiza mila, desturi na tabia za makafiri na kuzisherehekea kama mfano siku hii inayoitwa 'Valentine day' (Siku ya Wapendanao).
Na baya zaidi na la kusikitisha sana ni kwamba sherehe hizi zinaenezwa katika njia mbali mbali za mawasiliano kama kutumiana kadi, barua pepe (e-mail), salamu katika simu za mkono. Hakika fitna hii humfanya Muislamu aharibu 'Aqiydah (Iymaan) yake kwa kudhani kuwa anafanya jambo la kawaida na hali ni jambo lisilo katika sheria ya dini yetu bali ni shirki kubwa na upotofu wa kufuata wanayoamini makafiri.


SIKU ya wapendanao huadhimishwa kila ifikapo tarehe 14 Februari ya kila mwaka.
Watu wengi wanaosherekea siku hii kwa Nchi za Afrika Mashariki ni vijana walio kati ya miaka 18 hadi 35.
Historia ya sikukuu hii inaanzia miaka mingi jijini, Roma, Italia ikiwa inahusishwa na mtakatifu Valentine au Valentinus aliyekuwa akiishi jijini humo katika karne hiyo.
Wakati wa maisha ya mtakatifu Valentine Roma ilikuwa ikitawaliwa na Kaisari, Claudius II, ambaye alipata hisia wakati huo kuwa askari mkakamavu na bora zaidi ni yule asiyekuwa na mke wala familia (kapera).
Claudius alilifanyia kazi wazo lake na aliamua kupiga marufuku ndoa zote kwa askari wa nchi hiyo, jambo ambalo halikukubaliwa na mtakatifu, Valentinus.
Hivyo Valentinus alichukua jukumu la kukaidi amri ile na kuendelea kuwafungisha ndoa kwa siri maaskari waliokuwa wakitaka kufungishwa ndoa.
Haikuchukua muda mrefu, taarifa zilimfikia mfalme, Claudius na alipopata habari hizo aliamuru kukamatwa na kufungwa gerezani na kisha Valentinus aliuawa kwa amri ya Kaisari.
Kuna taarifa zinadai kuwa kabla ya kuuawa kwa Valentine wakati huo akiwa amefungwa, mtakatifu Valentine aliandika barua ya salamu kwa binti aliyekuwa amekwenda kumsalimia gerezani.
Na mwisho wa barua kulisomeka maneno yaliyoandikwa ‘From your Valentine.’
Tangu hapo Valentine akawa anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na siku hii ikawa inaadhimishwa duniani kote.
Baada ya kufariki kwa mtakatifu huyo ndipo wananchi wengi duniani wakaamua kuadhimisha siku hii kama sherehe ya kumkumbuka Mtakatifu Valentinus.
Namna sherehe hii inavyosherehekewa hivi sasa
Katika nyakati zetu hizi siku ya wapendanao au siku ya mtakatifu Valentine inayosherehekewa Februari 14 ya kila mwaka na watu wengi duniani, wakazi wa Nchi za Magharibi husherehekea siku hii kwa kutumiana kadi zenye maandishi ya Valentine, maua mekundu yanayoonyesha ishara ya mapendo.
Watu wengi wamekuwa wakiisherehekea kwa kula pamoja ikiwa ni pamoja na kutumiana kadi.
Mapambo ambayo yamekuwa yakitumika katika sherehe hizi ni yale yaliyotengenezwa katika umbo la moyo ikimaanisha mapendo ya kweli.
Maendeleo ya kutumiana kadi yalianza tangu karne ya 18, ikawa kama mtindo ulioonekana kupata umaarufu zaidi hadi ilipofikia karne ya 19 katika nchi za Uingereza.
Katika nchi ya Marekani na Amerika ya Kusini mtindo huu wa kutumiana kadi ulishika umaarufu kwenye karne ya 19 wakati huo ikifanywa kama moja ya sherehe kubwa nchini humo.
Wakati ukiingia Marekani wafanyabiashara wakubwa wa kadi katika nchi hiyo walifanikiwa kuuza zaidi ya kadi bilioni moja ndani na nje ya nchi hiyo, idadi iliyoikaribia ya uuzaji wa kadi za Siku kuu ya Krismasi.
Wengi wa watu ambao wamekuwa wakionekana kuisherehekea siku hii wamekuwa wakifikiria kuwa ni siku ambayo maalum ya uzinifu na kufanya uasherati, kumbe sivyo.
Nchi ya China, wananchi wake husherehekea siku hii kwa kupeana zawadi ya chokoleti, maua kwa wanawake ambao wanawapenda na wamekuwa wakiita kwa jina la pinyin.
Japan sikukuu hii inajulikana kama Tanabata, ambako wao huisherehekea Julai 7 kila mwaka.
Kwa upande wa nchi ya Saudi Arabia mwaka 2008, walichukua jukumu la kuchoma kadi zote za Valentine katika maduka yaliyoziingiza katika nchi hiyo, wakiwa wanashutumu kuwa siku hiyo ni maalumu kwa ajili ya Wakristo na si kwa Waislam.

Friday, 12 February 2010

siku ya tano ya mafunzo.

Mafunzo ya siku tano nipata kujifunza mambo mengi yakiwemo kufungua blog na kuweza kupata njia nyengine mbadala ambayo itanisaidia kupata mawasiliano na wandishi wengine wa Zanzibar na nje ya Zanzibar.
Mafunzo hayo yataweza kunisaidia katika kazi zangu mbali mbali za habari.

ENEO LA FORODHANI.


Eneo la bandari ya Zanzibar maeneo ya Forodhani mjini Zanzibar.
Hayo ni mazingira ya bahari ya Zanzibar bahari yake yanavyovutia.
Hii ndio haiba ya bahari ambao kuna upepo mwanana wa bahari ambao unanukia marashia ya karafuu.
Hali hii huvutia wengi wanapopata fursa ya kutembelea Zanzibar ili kuona mazingira ya Zanzibar na utamaduni wa watu wake jinsi walivyowakarimu sana.
Ukitaka kuyajua yote hayo harakisha kupata fursa ya kuja Zanzibar ili uweze kuthibitisha hayo niliyokueleza.

Ilivyokua Zanzibar hali halisi ndio hiyo hapo.


Enzi za ukoloni jinsi watu walivyokuwa wakiteswa, hali ilikuwa ni kweli na sio ya kubuni.
Hivi ndivyo ilivyokuwa Zanzibar ya zamani na sio ya sasa.
Kila unaposikia Zanzibar jenga taswira kama hii ndivyo ilivyokuwa.
lakini sasa Zanzibar tumshukuru M/Mungu kwa utulivu na amani iliyopo nchini.
picha hii ni baadhi ya maeneo ya watumwa yaliyopo katika Kanisa la Mkunazini mjini Zanzibar.