Thursday, 11 February 2010

JERRY MURO


JERRY MURO NI MWANDISHI WA HABARI WA ZAMANI KIDOGO AMBAE KWANZA ALIFANTIA KAZI KATIKA KITUO CHA TELEVISION CHA ITV NA HADI SASA ANAFANYIA KAZI KATIKA KITUO CHA TELEVISION CHA TBC. AMBAPO SASA ANAKABILIWA NA TUHUMA YA UTAPELI NA KESI IKO MAHAKAMANI LAKINI YUKO NJE KWA DHAMANA.

HALI YA SASA YA JERI MURO NI HII:-
Mwanahabari wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1), Jerry Muro, na wenzake wawili, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, na kusomewa mashtaka ya kuomba rushwa ya sh milioni 10 kutoka kwa Michael Wage Karoli ambaye alikuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

Mbali na mwanahabari huyo anayetetewa na wakili wa kujitegemea, Pascal Kamala, washtakiwa wengine ni Edmund Kapama na Deogratius Mgasa.

Huku wakishuhudiwa na umati wa watu, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo majira ya saa sita mchana wakiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi waliotanda pande zote za mahakama hiyo.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Gabriel Milumbe, Wakili Kiongozi wa Serikali, Stanslaus Boniface, akisaidiana na Wakili Kiongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Lincoln, walidai kuwa kesi hiyo ina mashtaka matatu.

Katika mashtaka hayo, Murro, ambaye kwa wiki nzima sasa ameibua mjadala mzito, anakabiliwa na mashtaka mawili wakati wengine wanakabiliwa na mashtaka yote matatu.

Wakili Boniface alidai kuwa shtaka la kwanza ni la kula njama kwa mujibu wa kifungu cha 32 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.

Alidai kuwa mnamo Januari mwaka huu, jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja, walikula njama kwa nia ya kutenda kosa linalohusiana na rushwa kinyume na kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.

No comments:

Post a Comment